JUMAMOSI: 24 OCTOBER 2015 –
UFUFUO
NA UZIMA MOROGORO
Na: STEVEN
NAMPUNJU (RP)
&
DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
Utangulizi:
Kwenye mji wapo watu wenye shughuli zao, makazi yao na ndipo watu wanaishi.
Wakoma kwa mujibu wa Biblia ni watu waliokuwa wanatengwa na jamii kana kwamba
wana laana ili kamwe wasiguswe na jamii yao. Mji unaweza kuwa umeharibiwa au
umetekwa. Mji wa Yeriko mfano, uliwahi kufungwa kabisa kwa ajili ya wana wa
Israeli. Upo uwezekano kabisa kwa mji kufungwa kabisa kwa sababu ya jamii
fulani. Maana yake, jamii iliyofungiwa nje haiwezi kuendelea hadi huo mji ukombolewe
kwa ajili yao katika Jina la Yesu.
Mji Wagerasi
pia ulikuwa siyo rahisi kuufikia kwa sababu ulifungwa ili watu wasiingie mle. Bahari
ilichafuka sana siku ile Yesu alipotaka kuelekea kwenye Mji huu wa Wagerasi.
Mtu huyo aliyewazuia watu kuingia humo alikuwa hakai nyumbani bali anaishi
makabaurini na kuzuia watu waliotaka kuipita njia ile kuelekea humo mjini. Yesu
aliyatoa mapepo yote yaliyokuwa yamemfunga huyu mtu na kumweka huru.
Imeandikwa katika LUKA 19:41-44…[Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, 42 akisema, Laiti ungalijua,
hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.
43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke;
watakuzingira na kukuhusuru pande zote; 44 watakuangusha chini wewe na watoto
wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya
kujiliwa kwako.]… Yesu aliuona Mji na kuanza kuulilia. Hata sasa
yamkini Yesu anaulilia mji wako, na kusema ”Laiti ungalijua ewe Morogoro, Laiti
ungalijua ewe Mwanza, Laiti ungalijua ewe Dar es Salaam,”. Yesu anauombolezea
mji ingawa wenyeji wa ule mji hawajui ni
kipi cha kufanya.
Mji unaweza kuutekwa na watu kwa maslahi fulani fulani. Mfalme hana mamlaka
tena kwa mji amboa tayari ulishatekwa na wenye nguvu.
Imeandikwa katika 2 WAFALME 6:24-33…. [Ikawa baada ya hayo, Benhadadi
mfalme wa Shamu akakusanya majeshi yake yote, akakwea akauhusuru Samaria. 25
Njaa ikawa kuu huko Samaria; na tazama, wakauhusuru, hata kichwa cha punda
kikapata kuuzwa kwa vipande themanini vya fedha, na kibaba cha mavi ya njiwa
kwa vipande vitano vya fedha. 26 Ikawa mfalme wa Israeli alipokuwa akipita
ukutani, mwanamke mmoja akamwita akisema, Unisaidie, bwana wangu, mfalme. 27
Akasema, Bwana asipokusaidia, nikusaidieje mimi? Ya sakafuni, au ya
shinikizoni? 28 Mfalme akamwambia, Una nini? Akajibu, Mwanamke huyu aliniambia,
Mtoe mtoto wako, tumle leo, na mtoto wangu tutamla kesho. 29 Basi, tukamtokosa
mtoto wangu, tukamla; nikamwambia siku ya pili, Mtoe mtoto wako, tumle; naye
amemficha mtoto wake. 30 Ikawa, mfalme alipoyasikia maneno ya huyo mwanamke, aliyararua
mavazi yake; (naye alikuwa akipita juu ya ukuta;) na watu wakaona, na tazama,
alikuwa amevaa magunia ndani mwilini mwake. 31 Ndipo akasema, Mungu anifanyie
hivyo, na kuzidi, kikimbakia kichwa Elisha mwana wa Shafati juu yake leo. 32
Lakini Elisha alikuwa akikaa nyumbani mwake, na wazee wakikaa pamoja naye; na
mfalme akamtuma mtu wa mbele yake; lakini hata kabla ya kufika kwake yule
aliyetumwa, akawaambia wazee, Je! Mwaona jinsi huyu mwana wa mwuaji alivyotuma
aniondolee kichwa changu? Angalieni, huyo aliyetumwa akifika, fungeni mlango,
mkamzuie mlangoni; je! Sauti ya miguu ya bwana wake haiko nyuma yake? 33 Hata
alipokuwa katika kusema nao, tazama, yule aliyetumwa akamshukia; naye akasema,
Angalia, mabaya haya yatoka kwa Bwana; kwani mimi kumngojea Bwana tena?]…Uwepo
wa njaa kali sana ulisababisha wamama wawili
kukubaliana kuzila nyama za watoto wao. Msaaada wa kweli unapatikana
katika Bwana aliyeumba mbingu na nchi. Haupo
msaada utakaopata kutoka kwa mbunge au hata rais. Kumbuka imeandikwa “Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye
mwanadamu”. Elisha alikuwa na uwezo wa kuzijua siri za mfalme wa Shamu
alizojadiliana akiwa chumbani kwake. Wakati mfalme anaapa kumwangamiza Elisha,
upande wa pili alikuwepo Elisha. Mungu ana uwezo wa kutupasha habari za siri
zinazopangwa vyumbani mwa adui zetu. Kuna watu ulioruhusu waingie ndani na
wakaleta madhara katika maisha yako. Ili muuaji asifanikiwe kukuchinja, njia
nzuri ni kumfungia nje.
Mwuaji anavyotumwa
kwako anakuja akiwa anajua sifa kuu mbili:
1.
Aliyetumwa
haendi peke yake, bali
huambatana na sauti ya miguu ya bwana wake nyuma yake.
Huu ni wakati wa kuwafungia nje wauaji wote ili
wasifanikiwe kuingia ndani na kutuchinja kwa Jina la Yesu. MARKO 16:19-20....[Basi Bwana Yesu, baada ya kusema
nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu. 20 Nao wale
wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na
kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.]…Yesu
alilithibiitisha neno lile kwa ishara ingawa alikuwa mbinguni. Na hata yule mfalme
alipomtuma kiongozi yule kwenda kwa Elisha, sauti ya miguu yake haikumuacha.
2.
Ukichukua
hatua, uwezo wa utiisho vinakutangulia. Ili ufanikiwe lazima
uwe na uthubutu. Imeandikwa katika LUKA
13:31-35…[Saa ile ile
Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali
pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua. 32 Akawaambia, Nendeni, mkamwambie
yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu
nakamilika. 33 Pamoja na hayo imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na
kesho kutwa; kwa kuwa haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemu.]….
Kumbe waliokuja kumwambia Yesu atooke pale kwenye wito wake, lengo lao
ni ili Yesu asitoe pepo na kuponya wagonjwa, asitimize wito wake.
Wapo watu wanaokuja kwako kana kwamba wanataka kukupa msaada lakini kumbe ni
kwa ajili ya kukutoa wewe kwenye wito wako. Kuna mahali pa kukaa na kufanyia kazi
ili ukombozi utokee lakini wengine hawataki ufanye hivyo.
UKIRI
Mahali popote ambapo kwenye mji wangu wa mafanikio
leo nakataa katika Jina la Yesu. Achia maisha yangu katika Jina la Yesu.
Amen.
|
Imeandikwa katika 2WAFALME 7:1- …[Elisha akasema, Lisikieni neno la Bwana; Bwana asema
hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na
vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria. 2 Basi yule akida,
ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu,
akasema, Tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili
lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini
hutakula.]…Kumbuka kuwa Mungu hupendezwa na watu wenye kuchukua
hatua.
Imeandikwa katika 2WAFALME 7:3-11…[Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji;
wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe? 4 Tukisema, Tutaingia mjini, mjini
mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya!
Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua,
tutakufa tu. 5 Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha
Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu. 6 Kwa
maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na
kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme
wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane
nasi. 7 Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao,
na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa,
wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao. 8 Basi wale wenye ukoma walipofika
mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua
fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika
hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha. 9 Ndipo
wakaambiana, Mambo haya tufanyayo si mema; leo ni siku ya habari njema, na sisi
tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende
tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme. 10 Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa
mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote
huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema
zao kama walivyoziacha. 11 Na mabawabu wakaita wakawaambia watu wa nyumba ya
mfalme.]…Majadiliano ya wakoma yalionesha kuwa, walikaa nje kwa muda
mrefu kwa sababu ya kutengwa na jamii.
Wakaona ni afadhali waliendee jeshi, kama nikufa wafe tu. Mji unakombolewa usiku na mapema, kabla ya alfajiri.
Majeshi ya Washami waliamua kutoroka. Waliokamata mi leo ni siku ya kuwakimbiza
kwa Jina la Yesu.
Usiogope kuchukua hatua kwa sababu yoyote ile: Kwamba haufahamiki, kwamba hauna cheo au jina kubwa. Wanaohatarisha maisha yao huwa
wa kwanza kufurahia matunda ya utajiri wa nchi yao.
Imeandikwa katika 2WAFALME 7:12-20… [Mfalme akaondoka usiku, akawaambia watumishi wake, Sasa nitawaonyesha
ninyi walivyotutendea Washami. Wanajua ya kuwa tuna njaa; basi wametoka
kituoni, ili kujificha kondeni, wakisema Watakapotoka mjini, tutawakamata hai;
tena tutapata kuingia mjini. 13 Na mmojawapo wa watumishi wake akajibu, akasema,
Kunradhi; baadhi ya watu na watwae farasi watano katika hao waliosalia,
waliobaki ndani ya mji (tazama wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli waliobaki
ndani yake; tazama, wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli walioangamia),
tukawapeleke tukaone. 14 Basi wakatwaa magari mawili na farasi zake; mfalme
akawatuma kuwafuata Washami, akasema, Enendeni, mkaangalie. 15 Wakawafuata
mpaka Yordani; na kumbe! Njia yote ilikuwa imejaa mavazi na vyombo,
walivyovitupa Washami, wapate kukimbia upesi. Watu wale waliotumwa wakarudi,
wakamwambia mfalme. 16 Basi watu wakatoka, wakaziteka nyara hema za Washami.
Ikawa kipimo cha unga mzuri kikauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri
kwa shekeli, sawasawa na neno la Bwana. 17 Naye mfalme akamweka yule akida,
ambaye alitegemea mkono wake, awasimamie watu langoni; na watu wakamkanyaga
langoni, akafa; kama alivyosema yule mtu wa Mungu, aliyenena hapo mfalme
alipomshukia. 18 Ikatukia kama vile yule mtu wa Mungu alivyomwambia mfalme,
Vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, na kipimo cha unga mzuri kwa shekeli,
ndivyo vitakavyokuwa kesho, panapo saa hii, katika lango la Samaria; 19 na yule
akida akamjibu mtu wa Mungu, akasema, Sasa tazama, kama Bwana angefanya
madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akasema, Angalia, wewe
utaliona kwa macho yako, lakini hutakula. 20 Ikampata vivyo hivyo, kwa kuwa
watu wakamkanyaga langoni, akafa.]…Mji unaweza kuwa ni wewe
mwenyewe. Kukiwepo na vurugu rohoni mafanikio hayawezi kuonekana. Unapoona mtu
hawezi kufanikiwa, upo uwezekano kuwa rohoni hakuna utulivu.
Ili ukombozi upatikane, usitegemee akili zako au uwezo wako. Hayupo ambaye aliwahi kushindana na kanisa au Mungu
mtu huyo akaishi. Walioshindana na Eliya na papo hapo wakaapa kumwangamiza
Elisha, hawakutimiza azma zao. Maisha yako ya kiroho ili ufanikiwe, ni
budi kuukomboa mji. Ni hadi palemji
unapoko,bolloewa na ndipo uhuru timilifu
uanpopatikana. Wanaotegemea akili zao hukanyagwa langoni. Leo kila akida wa
kiroho anayezuia chakula kisitokee katika mji wako akanyagwe na kuangushwa
katika Jina la Yesu.
Wewe ambaye hujaokoka leo ni siku njema kwako
kutengeneza maisha yako na Yesu kwa kumpokea Yesu moyoni mwako.
=== © Information & Media Ministry ===
(Ufufuo Na Uzima -
Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Church
Leadreship:
Bishop Dr. Godson Issa
Zacharia
(Glory of Christ
(Tanzania) Church in Morogoro)
Cellphone: (+255)
765979866 /or +255 713459545