Sunday, September 14, 2014

SOMO: KUZIFUNGUA KAMBA ZA MAUTI-Na: Dr. Godson Issa Zacharia (SNP)

JUMAPILI: 14 SEPTEMBER 2014 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO


Utangulizi: Somo la Jumapili ya leo linaitwaKuzifungua kamba za mauti”. Shetani na wasaidizi wake hapa duniani kazi zao kuu ni kufanya uwakala wa mauti. Watu wanapofungwa kamba za mauti, umauti huingia ndani mwao. Wanaofunga kamba hizi hulenga  mauti hii ikae ndani mw mtu waliyemkusudia.


Baba (SNP Dr. Godson) akiwa amezama rohoni,
Jumapili 14/09/2014 katika Nyumba Ya Ufufuo na
uzima -Morogoro.
LUKA 4:18-19…[Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao,  Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.]…. Haya ni maneno ya  Yesu aliyoanza nayo akiwa hekaluni. Vivyo hivyo, katika hali za kawaida, mtu anapokuwa anaandika au kuongelea jambo fulani,  huanza kwa kutoa muhtasari (Abstract) ya hilo jambo. Kuhubiria maskini  habari njema maana yake, endapo ulikuwa huzai, unatangazia kupata watoto, asiye na kazi unatangaziwa kupata kazi; Waaliofungwa kufunguliwa; wale waliowahi kuona na kukosa kuona,wanatangaziwa kupata kuona tena vile vilivyokosa kuonekana maishani mwao;


Baba (SNP Dr. Godson akimhoji Lucas, mtoto aliyepotea
na kuibukia kuzimu alhamis 11/09/2014. Ushuhuda huu upo
tayari kwenye hii Blog ya ufufuo na Uzima -  Morogoro.
Wale wote wasiopenda kusikia mambo ya uzima, ni  mawakala wa mauti. Mfano mmoja wapo kibiblia ni  pale ambapo  watu walikuwa wakihudhuria mkutano wa Yesu, lakini  lengo lao likiwa ni kutaka kumua Lazaro ambaye Yesu alikuwa hapo awali ameshamfufua.


Habari njema ni kuwa waliofungwa na kamba za mauti leo hii watawekwa huru na kufunguliwa kwa Jina la Yesu.  Lengo la kufungwa na kamba za mauti ni kusababisha kifo; kifo katika uwezo wako wa kuomba, kifo cha uwezo wa kumtumikia Mungu,  kifo cha uwezo wa kufanya kazi n.k.


Baba (SNP Dr. Godson akimhoji mama wa Lucas, mtoto
aliyepotea na kupatikana kesho yake. Ushuhuda huu upo
tayari kwenye hii Blog ya ufufuo na Uzima -  Morogoro.
MARKO 7:31-35 [Akatoka tena katika mipaka ya Tiro, akapita katikati ya Sidoni, akaenda mpaka bahari ya Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli. 32 Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye utasi, wakamsihi amwekee mikono. 33 Akamtenga na mkutano faraghani, akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi, 34 akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka. 35 Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri.]…. Kwa hiyo ulimi wa huyu mtu ulikuwa umefungwa kamba ambazo hazionekani kwa namna ya macho ya mwilini, lakini kamba zilikuwepo katika ulimwengu wa roho. Kamba hizi huitwa 'kamba za mauti'. Kizazi cha mtu chaweza kufungwa na mtu wa aina hii hawezi kamwe kupata ujauzito. Ukitaka kufunguliwa ni kuamuru mamlaka ya Jina la Yesu ili ufunguliwe na kuwekwa huru. Shetani ni 'Bwana Jela' ambaye mara zote hapendi kuwaachia wafungwa wake wawe huru. Unaweza kuona mtu  hazai  mtoto, kumbe ipo sababu za rohoni ambapo unamkuta mtu wa aina hii amefungwa kamba za mauti.


ISAYA 14:17…[Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao? ]… Ulimwengu unaonekana kama una watu kumbe hao siyo watu ila ni 'sura za watu'.


MAOMBI: Naikatakata kamba ya kichawi iliyonifunga maishani mwangu kwa Jina la Yesu. Amen.


1 WAFALME 22:20-23… [Bwana akasema, Ni nani atakayemdanganya Ahabu, ili akwee RamothGileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi. 21 Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi nitamdanganya. 22 Bwana akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo kinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka ukafanye hivyo. 23 Basi angalia, Bwana ametia pepo wa uongo kinywani mwa manabii wako hawa wote; naye Bwana amenena mabaya juu yako.]… Kupitia andiko hili,  tunaona kuwa shetani anayo tabia ya ‘kwenda na kuwa’. Kwa hiyo shetaani akitaka usiweze kusema, atakuja na kuwa 'pepo la ububu'. Akitaka mtu asiweze kutembea,  atageuka na kuwa 'kama zege' miguuni mwa huyo mtu,  na kufanya usiweze kutembea kabisa.  Kumbuka jinsi Ayubu alivyopata majipu. Shetani anaweza kugeuka na kuwa 'pepo la hasira', na kumfanya mtu awe na hasira kali sana saa zote. Shetani anaweza kugeuka na kuwa 'pepo la hasara', na matokeo yake mtu akiingiliwa na pepo la aina hii hawezi kupata faida kwa kazi yoyote aifanyayo.


Chanzo kikubwa cha watu kufungwa na kuwekwa gerezani ni  'DHAMBI'. Ukitaka kuishi vizuri, kataa kutenda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Dhambi husababisha mtu  kuwa mtumwa (YOHANA 8:34….. Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.). Kataa dhambi ili usiwe mtumwa wa shetani.


MAOMBI: Kuanzia leo,  Naacha dhambi kwa Jina la Yesu. Amen


Baadhi ya Makutano waliohudhuria ibada Jumapili 14/09/2014
katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro
ZABURI 18:4…[Kamba za mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.]…Ina maana Daudi alikuwa anatembea kama wewe na mimi lakini tayari katika ulimwengu wa roho Daudi amejiona akiwa amefungwa kamba za mauti.



ZABURI 116:3….[Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni;]...Pindi ufungwapo kamba za mauti, shida za kuzimu zitaanza kukufuata. Kamba za mauti ni 'ishara ya  kifo'. Sanda vivyo hivyo,  huvishwa watu wanapokuwa wamepoteza uhai wao (wafu).  Endapo watoto wako watakuwa wamefungwa kamba za mauti, utakuta kuwa,  wale waliowafunga wameshawafanya 'maiti' ingawa wanatembea. Kwa hiyo, mtu anakuwa hai kimwili lakini katika ulimwengu  wa roho mtu huyo walishamuua na hata pengine walishaadhimisha ‘arobaini’ ya huyo mtu bila yeye kujua!!!.


YOHANA 11:38-43… [Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake. 39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. 40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? 41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. 42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. 43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.  44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.  ]… Yamkni wewe unajiona kuwa tayari umeshaokoka, lakini kamba za miguuni bado zipo na hazijafunguliwa  ili uweze 'kupiga hatua'. Wajanja wanaweza kukufunga sanda katika ulimwengu wa roho. 'Sanda' inawakilisha 'mauti'. Ni kweli umeokoka tayari, lakini yawezekana pia kuwa katika hatua zako za maendeleo zipo kamba tayari zimefungwa kukurudisha. Unaanza masomo, masomo yanharibika. Unaaaza biashara, biashara inaharibika.


Showers of Glory wakimwimbia Bwana Yesu, tar. 14/09/2014,
ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima- Morogoro.
MAOMBI: kwa Jina la  Yesu , Ewe sanda uliyefungwa kwenye hatua zangu za maendeleo, funguka, sanda iliyofunga elimu yangu, sanda iliyofunga sura yangu isionekane, nakuamuru funguka na uondoke kwa Jina la  Yesu. Amen



© Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
==(Cellphone: (+255) 713 45 95 45)==



Share:
Powered by Blogger.

Pages