THIS IS MY STORY -
JUMAPILI 14.09.2014
Lucas akihojiwa na Baba (SNP Dr. Godson), akishuhudia jinsi ambavyo alipotea na kwenda hadi Kuzimu. Kushoto aliyesimama ni mama mzazi wa Lucas (Maria Jumamos). |
Utangulizi: Mtoto Lukas ana umri
miaka 8, yupo darasa la pili, alipotea jioni ya saa kumi na moja siku ya Alhamisi wiki
hii (11/09/2014) baada ya kwenda kuchota
maji na dada yake, lakini maajabu dada
alirejea nyumbani bila kuwa na mdogo
wake.
Nyumbani walimsubiri kidogo na kuanzia
saa moja usiku msako wa kumtafuta ukaanza rasmi. Msako huu uliongozwa na Mama mzazi wa Lucas aitwae Maria
Jumamos (Potential Shepherd) kwa kupita na kuuliza majirani zake, nyumba
hadi nyumba na kutoa taarifa ili kama wapo watu waliomuona huyu mtoto wamsaidie
kumjulisha lakini bila mafanikio.
Maelezo ya mama mzazi: Alhamisi 11/09/2014
Lucas akihojiwa swali kuhusu alivyokutana na 'Kivuli Jini' |
Muda wa saa tano usiku, mama huyu alimpigia simu Baba (SNP Dr. Godson) na kumweleza kilichotokea, huku akilia. Baba alimtuliza na kuyafanya maombi mafupi, kwa kuamuru malaika wafanye msako wa nyumba hadi nyumba ili kumrudisha Lucas. Baada ya maombi haya alimwambia huyu mama wa Lucas alale bila hofu na kumsubiri mwanane kwani hakika atarejea kesho yake akiwa mzima.
Kesho yake: Ijumaa
12/09.2014
Mama wa Lucas alitii maelekezo aliyoambiwa na
muda wa saa kumi na mbili alfajiri aliamka
na kwenda kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kilimanjaro – Kihonda,
Morogoro), kuhusu upotevu wa Lucas.
Huyu mwenyekiti (ambaye pia kitaaluma ni
mganga wa kienyeji) alimuhoji mama wa Lucas baadhi ya maswali kuulizia taarifa binafsi
muhimu kama vile jina lake, kabila lake
n.k. Baadae kiongozi huyu alimwambia mama wa Lucas kuwa jana yake taarifa zilimfikia
za mtoto aliyeokotwa hapo mtaani, ila watu walioleta taarifa hizo hakuwataja majina yao. Anachodai ni kuwa hao watu waliondoka zao lakini huyo mtoto hakuachwa pale nyumbani.
Mwenyekiti wa Kitongojji alimuonesha mama wa
Lucas viatu aina ya 'yeboyebo' na kumwambia huyu mama aende zake nyumbani kuendelea
kumtafuta huyu mtoto na pindi akimpata azilete taarifa hizo kwake. Mama wa Lucas
alimshangaa sana huyu kiongozi, kwani badala ya kumpatia jibu la wapi alipo mwanae, badala yake yeye alimpatia viatu vya ‘yeboyebo’‼!
Mama wa Lucas (kushoto) akihadithia yaliyomkuta mwanae (aliyesimama kulia). Katikati ni Baba (SNP Dr. Godson) wakatiwa ibada ya Jumapili 14/09/2014. |
Wakati huyu mama anarudi nyumbani kwake na
zile yeboyebo, ndipo alipopigiwa simu
upya na baba (SNP Dr. Godson) aliyeendelea kumsihi aendelee kupiga
majeshi, na kwamba hata yeye binafsi
anamwombea na kumwamini Mungu kuwa huyo mtoto atapatikana tu
akiwa hai.
Rafiki wa mama mzazi wa Lucas (Agatha Thadey) akieleza yale aliyoshuhudia kumhusu Lucas alipokutwa nyumba ya mwenyekiti wa Kitongoji, leo tarehe 14/09/2014 Ufufuo na Uzima Morogoro. |
Hata hivyo, alipofika karibu na nyumbani, alikutana na rafiki yake aiwae Agatha Thadey (Potential Shepherd) mbaye pia ni majeshi majeshi wa Ufufuo na Uzima - Morogoro. Huyu baada ya kusikia maelezo ya taarifa ya kupatikana tu kwa yeboyebo za Lucas bila mwenye viatu hivyo kuonekana, kwa ujasiri alimtia moyo huyu mama na kumwambia kuwa ‘haiwezekani, kwani aliyekupatia hizi yeboyebo ndiye mwenye majibu ya alipo Lucas na lazima huyo mwenyekiti ahusike moja kwa moja na maelezo ya alipo huyu mtoto . Aliongeza kusema ‘iweje viatu viwepo lakini mwenye viatu haonekani??!’ Waliondoka pamoja na kurudi kwa huyo mwenyekiti wa kitongoji huku wakifanya maombi ya kushindana.
Taarifa za kuonekana kwa mtoto
wa ajabu mtaani - Ijumaa 12/09/2014
Walipokaribia nyumbani kwa huyu mwenyekiti, njiani,
walikutana na baadhi ya majirani waliokuwa wakihadithiana kuhusu tukio la
kuonekana kwa ‘mtoto wa ajabu’ hapo mtaani kwao‼! Kwa mujibu wa hao majirani,
kwenye ile nyumba ya mwenyekiti wa kitongoji kuna mtoto ambaye ameonekana anapita
kwenye dari, na anapanda ukuta mithili ya mjusi na kupenya kwenye vitundu vidogo
vidogo sana ambayo kwa hali ya kawaida ‘mwanadamu wa kawaida’ hawezi kufanya
hivyo.
Hii ikawa fursa ya mama wa Lucas na rafiki
yake kuwaeleza kuwa wanachosema ni ‘mtoto wa ajabu’ siyo kweli, bali atakuwa ni
huyo mtoto wao LUCAS wanayemtafuta. Basi wakaelekea moja kwa moja kwa ile
nyumba ya mwenyekiti wa kitongoji, ambapo
walikuta halaiki ya watu wakimshangaa Lucas, huku wakihadithiana yaliyotokea,na
vituko vya huyo aitwae ‘mtoto wa ajabu’.
Walipofika walimuona Lucas akiwa ameshakamatwa huku amebadilika
sura na amevimba usoni‼! Inasemekana kuwa katika zile harakati za kumkamaata, walitumia fimbo. Hata hivyo, Maajabu ni pale Lucas alivyokuwa akibadilika
sura na rangi yake kila baada ya muda mithili ya kinyonga. Mama wa Lucas na
rafiki yake walichochea maombi ya kushindana kuharibu nguvu za giza zilizokuwa
zinamshikilia Lucas na hatimaye ufahamu
wake ukamrudia.
Wakati hayo yakiendelea huyo mwenyekiti
alikuwa keshaondoka nyumbani kwake. Alipigiwa simu na akaja mara moja. Hata hivyo,
pindi alipofika alianza kugomba na kulalama kuwa ingawa huyu mtoto ni mdogo lakini amemshinda nguvu‼!, Aliongea
kwa ukali, akiwaamuru wazazi wa Lucas kumgharamia nauli ya bodaboda aliyokodi
kurudi nyumbani, na kuwataka wakeshaondoka baadae warudi kutengeneza zile sehemu za nyumba yake ambapo Lucas aliziharibu
wakati akipenya na kutambaa kama mjusi kwenye kuta na dari za ile nyumba.
Ni yapi Maelezo
binafsi ya Lucas ya kilichomtokea?
Baada ya Lucas kupatikana na kuwa na ufahamu
wake, leo hii ameeleza kile kilichotokea mbele
ya mamia ya majeshi ya Bwana wa Ufufuo na Uzima Morogoro. Kwa mujibu wa maelezo
yake, mambo yalianza pale alipoenda kuchota maji na dada yake. Wakati wa kurudi
kutoka kisimani, Lucas alijiongoza mwenyewe kwa kupita njia tofauti na dada
yake. Njiani ndipo alipokiona kivuli na alipokikanyaga tu, hatimaye kile kivuli kilimshika mkono na kumvuta na kumwelekeza
njia hadi alipojikuta yupo kuzimu. Kwa maneno ya Lucas, kile kivuli
kumbe kilikuwa ni “jini.”
Kile kivuli kilimpeleka Lucas hadi mahali mkuu wa sehemu ile (Shekhe Abduli)
anapoishi. Huyu Shekhe alimnywesha Lucas damu ya wanadamu kiasi cha nusu dumu
wakati wakiwa wote huko kuzimu‼!!
Ni kwa nini Lucas alinyweshwa hii damu?
Huyu shekhe Abduli alimnywesha Lucas hiyo
damu ili atakapomtuma kazi apate nguvu kuwashinda maadui zake. Mmojawapo wa maadui
hao waliolengwa kudhuriwa ni mwenyekiti wa kitongoji kile. Lucas
alitumwa aipeleke dawa ambayo akifika tu kwa huyo mwenyekiti wa kitongoji angeimwaga
kwenye ile nyumba yake, na baadae mwenyekiti huyu apende asipende lazima angekufa‼!!
Lucas aliwezaje kwenda
kwa mwenyekiti wa kitongoji kutimiza lengo hili?
Lucas anasema,aliporudishwa juu akitokea kule
kuzimu, alikutana na watu aliowaita ni ‘Maustaadhi wa Dukani’ pale mtaani kwao.
Hawa ndio waliojifanya ‘wasamaria wema’ kwa kumpokea na kutengeneza mbinu ya kuwahadaa
watu kuwa kuna mtoto wamemuokota‼
Lengo la wao ‘kumuokota’ lilikuwa ni mtego uliotengenezwa ili kumfikisha Lucas kwa
huyu kiongozi wa serikali aliyekusudiwa kudhuriwa na ile dawa kutoka kuzimu bila
yeye kujua‼. Walisingizia kuwa huyu mtoto Lucas ameokotwa na haijulikani
anapokaa na ndipo fursa ya kwenda kwa nyumba ya mweyekiti wa kitongoji
ikatokea. Walimfikisha Lucas kwa mwenyekiti wa Kitongoji na wakatoa maelezo ya tukio la mtoto aliyeokotwa, kisha hawa
‘maustadhi wa dukani’ ghafla waliondoka na kurudi kwao. Kumbe kuondoka kwao kulisababisha yule ‘kivuli
jini’ wa kuzimu amfiche Lucas kwenye magunia ya mahindi ya ile nyumba ya
mwenyekiti wa kitongoji, ili kufanikisha ule mpango wa ile dawa ya Shekhe Abduli. Ndiyo
maana haikuwa rahisi kwa mama mzazi wa
Lucas au hata mwenyekiti wa kitongoji mwenyewe kuweza kumuona Lucas pale
alipokuwa ameachwa au kufichwa.
Ilikuwaje hata Lucas
anig’ginie kama nyoka na kupita kwenye matundu?
Lucas anasema, yule ‘jini kivuli’ ndiye aliuleta mwili mwingine tofauti na ambao ndio
Lucas alioutumia kujificha na kupita kwenye matundu madogo madogo. Jini huyu
alikuwa akimhadaa Lucas kumwambia eti ni yeye rafiki yake mpendwa.
Lucas anazungumzia je
Maisha yalivyo kule Kuzimu?
Lucas anasema watu waliokuwepo huko kuzimu ni wengi kuliko hata waliofika ibada
ya hapa kanisani leo Jumapili 14/09/2014.
Anasema hao watu walikuwa wamevalia vichupi tu.
Tukio la Lucas limetafsiriwa je hapo mtaani?
Lucas akielezea maisha yalivyo huko kuzimu, leo 14/09/2014 katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima Morogoro. |
Majirani walikiri kuwa wapo watoto ambao wamepotea kwa mazingira ya kutatanisha siku za karibuni kwenye kitongoji hicho hicho bila kupatikana na ndiyo maana inawashangaza kuona mtoto huyu Lucas ameweza kupatikana akiwa salama. Sifa na Utukufu Apewe Bwana Yesu Kristo. Amen.
MAOMBI: Kwa Jina la Yesu, Nawapiga majoka wote walionizingira katika Jina la Yesu. Ninaamuru majini wote waliokaa ndani ya mtu, au ndani yangu waondoke, na kuwaagiza waachie na kumkimbiza huyu mtu na kumleta mara moja, kwa Jina la Yesu. Amen.
© Information Ministry
(Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
==(Cellphone: (+255) 713
45 95 45)==