JUMAPILI: 12 OCTOBER 2014
- UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi: Somo la Ibada ya leo linaitwa “Aliyetumwa Kuzifungua Kamba
Amefika”. Leo tunakamilisha masomo ya semina yetu iliyoanza wiki jana kuhusiana
na kizikata kamba zilizofungwa na ndugu wa karibu. Kufungwa (kwa kiiingereza 'incapacitation') maana
yake ni kuondoshwa kwa uwezo wako wa kufanya kile ambacho Mungu anataka uweze
kukifanya: mathalani mtu wa kuolewa hatawaweza kuolewa, mtu wa kufanya kazi hatoweza kufanya kazi n.k.
Leo ni siku ya 7 ya hii semina, na katika Biblia, namba 7 ni ishara ya ukamilifu. Mtu mmoja
aitwae Naaman, aliambiwa na mtumishi wake kuwa
endapo atasafiri na kwenda kwa
Nabii wa Israeli, ukoma wake ungetoweka. Lakini hata hivyo, Nabii wa Mungu hakuja kumuona Naaman, bali alitoa tu maagizo
kwamba Naamani adumbukie mara 7 katika
maji ya mto Yordani, na alipomtii,
alipata uponyaji wake siku ile ile. Ukuta wa
Yeriko nao ulianguka baada ya maombi ya kuuzunguka ukuta
huu kwa muda wa siku 7. Mungu aliiumba dunia yote hii na kupumzika ilipofika siku ya 7. Yote haya yanaoonesha kuwa, siku ya 7 ni muhimu sana kwa kufikia ukamilifu.
Majeshi ya Bwana yakisikiliza kwa Makini Somo la siku ya leo 12/10/2014, Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro |
ZABURI
18:4… [Kamba za mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.]…
Kuna kamba, siyo kama zile za 'katani' au 'manila' au 'kudu' ulizozoea kuziona. Ni kamba
za rohoni, zitokazo kuzimuni, ni mashetani na mapepo na mizimu yasiyoonekana kwa macho. Wachawi wanao uwezo wa kishetani wa kumfunga mtu ili asiwe na uwezo wa kufanya jambo lolote.
Endapo kamba zimekuzunguka, kila jambo utakuwa unajaribu jaribu tu kufanya bila
mafanikio ya kukifanya hicho kitu kwa ukamilifu. Unapofungwa kamba za kuzimu, ujue shida za
kuzimu lazima zikufuate. Utahangaika kwa
madaktari wote bila kupona, utajaribu kusoma shule zote bila
mafanikio.
ZABURI
18:5…[Kamba za kuzimu zilinizunguka, Mitego ya mauti
ikanikabili.]… Kumbe zinapokuwepo kamba, 'mitego' nayo hujitokeza. Yesu
alipokuja duniani, kabla ya kuanza
huduma yake alijitambulisha kwa kutoa ufupisho wa kazi yake kwa kusoma neno la
Mungu kutoka Isaya 61, kama
ilivyoandikwa:- LUKA
4:17-19….[Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo,
akatafuta mahali palipoandikwa, 18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana
amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia
wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu
kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 19 Na kutangaza mwaka wa Bwana
uliokubaliwa.].. Yesu alisema haya kwa sababu anajua
anayewafunga watu kwa kamba za kuzimu hapendi kuwaachilia watu waende zao huru.
Showers of Glory - Ufufuo na Uzima Morogoro, wakiwa kwenye harakati za kumwimbia Bwana Yesu leo 12/10.2014 |
Yamkini yupo
mtu ambaye hapendi kufanya uzinzi, lakini kila amuonapo mwanamke, hali ile ya kutenda uzinzi inamjia. Leo ni siku maalumu ya kuzikata hizo
kamba kwa Jina la Yesu. Yamkini yupo mtu ambaye mara zote ni mwizi au muongo. Hizi
ni kamba zitokazo kuzimu,inapaswa
zikatwe leo zote kwa Jina la Yesu.
ISAYA 14:17…[Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?]…Kamba zikeshafungwa kutoka kuzimu yule anayezifunga (shetani) hapendi kuachilia huru hao watu/wafungwa ili warudi katika hali zao za awali. Endapo kamba ni ya umaskini, ukijaribu kufanya biashara, shetani atazidi kuzikaza hizo kamba kwa sababu anajua ukiendelea tu na biashara utatoka kweye hiyo hali ya umaskini. Kamba nyingine hapa Tanzania zilikuja kwa mtindo wa DECI hadi makanisani. Baadhi ya walokole bila kujua 'ule ni mtego wa shetani', wakaingiza mamilioni ya fedha zao humo. Wakawa na msemo usemao ‘tunapanda na kuvuna maradufu’ ili kuondoa umaskini. Ghafla wanamaombi walipoomba, ile kamba ikakatika na mwishowe, DECI ikafungwa, wahusika wote wakuu wa DECI wakafungwa jela, na pesa yote ikshikiliwa na serikali hadi leo!!!.
MAOM
BI:
Naamuru Kamba ya umaskini
ikataike kwa Jina la Yesu. Amen
|
Yupo mmoja tu anayeweza kuzikata kamba walizofunga mashetani katika maisha yako. Wanaosanifu hizi kamba (designers) hudhani kuwa hakuna wa kuzikata hizo kamba. Yesu alizikata kamba nyingi sana, kwa kuweka huru watu waliokuwa na mapepo, kuwapa uwezo wa kuona waliokuwa vipofu, kuwaponesha wagonjwa na hata kuwafufua waliokuwa wamekufa, akiwemo Lazaro.
IMEANDIKWA:-
(A) MARKO
11:1-7….[Hata walipokaribia Yerusalemu karibu na Bethfage na
Bethania, kukabili mlima wa Mizeituni, aliwatuma wawili katika wanafunzi wake, 2
akawaambia, Nendeni mpaka kile kijiji kinachowakabili; na katika kuingia ndani
yake, mara mtaona mwanapunda amefungwa, asiyepandwa na mtu bado; mfungueni,
kamleteni. 3 Na mtu akiwaambia, Mbona mnafanya hivi? Semeni, Bwana anamhitaji
na mara atamrudisha tena hapa. 4 Wakaenda zao, wakamwona mwanapunda amefungwa
penye mlango, nje katika njia kuu, wakamfungua. 5 Baadhi ya watu waliosimama
huko wakawaambia, Mnafanya nini kumfungua mwanapunda? 6 Wakawaambia kama Yesu
alivyowaagiza, nao wakawaruhusu. 7 Wakamletea Yesu yule mwanapunda, wakatandika
mavazi yao juu yake; akaketi juu yake.]…
(B) MATHAYO
21:1-10…[Hata walipokaribia Yerusalemu, na kufika Bethfage,
katika mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu alipotuma wanafunzi wawili akiwaambia, 2
Enendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mara mtaona punda amefungwa, na
mwanapunda pamoja naye; wafungueni mniletee. 3 Na kama mtu akiwaambia neno,
semeni, Bwana anawahitaji; na mara huyo atawapeleka. 4 Haya yote yamekuwa, ili
litimie neno lililonenwa na nabii, akisema,
5 Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, naye
amepanda punda, Na mwanapunda, mtoto wa punda. 6 Wale wanafunzi wakaenda zao,
wakafanya kama Yesu alivyowaamuru, 7 wakamleta yule punda na mwanapunda, wakaweka
nguo zao juu yao, naye akaketi juu yake. 8 Watu wengi katika ule mkutano
wakatandaza nguo zao njiani; na wengine wakakata matawi ya miti, wakayatandaza
njiani. 9 Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti,
wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la
Bwana; Hosana juu mbinguni. 10 Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote
ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu?]…
Maandiko yote mawili hapo juu yanazungumzia habari moja. Ni kweli kuwa 'punda na mwanapunda' si mali ya Yesu, lakini wapo watu waliomfunga na kama wanafunzi wa Yesu
wangeulizwa kwa nini wanamfungua walipaswa
kujibu “Yesu ana haja naye”. Yesu anafahamu mahali pale ulipofungiwa. Anafahamu
kila kitu na hata wale waliokufunga anawajua.
Hawa wameokoka!!! Wameamua kwa hiari yao na kaili zao timamu, kumpa kisogo kibogoyo (shetani) na kumfuaata Yesu Kristo leo 12/10.2014 |
Imeandikwa 2 KORINTHO 4:3-4….“Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika
kwa hao wanaopotea; 4 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao
wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake
Mungu”]…. Hizi zote ni aina ya kamba ambazo zinashikilia 'akili' za watu, hata wanapokuwa na shida hawapo tayari kuja
kwa Yesu ili shida zao ziondolewe. Watu wa aina hii hutumia taaluma zao kujisifu, kwa kujiona wasomi basi
hawataki kabisa kumuamini Yesu Kristo ambaye ndiye mwenye uwezo wa kuzikata kamba za
matatizo yao.
Yesu anakijua kijiji
ulichofungiwa. Yesu Kristo anataka kukifungua hicho kifungo chako
kwa kuwa hata aliyekufunga Yesu Kristo
anamfahamu. Yesu anakiona kifungo ambacho wewe na mwanao mmefungwa pamoja kama yule punda na mwanapunda walivyokuwa.
Wapo pia walinzi wanaokaa kulinda kifungo hiki:- MARKO11:3…[Na mtu akiwaambia, Mbona mnafanya hivi? Semeni,
Bwana anamhitaji na mara atamrudisha tena hapa.]…Wasimamizi wa
kifungo huwekwa. Wamewekwa watu kabisa ili
wewe ukae katika kifungo chako
kwa kipindi chote cha maisha yako.
MAOMBI:
Leo Nakwenda, walikofungia biashara yangu. Nakwenda wawlikofimngia ndoa yangu,
Nakwendaaaaaaaa Kwa Jina la Yesu. Amen
|
Wasimamizi wa kifungo wapo makini mno. Hawa waliwahi hata kumsimamia Yesu akiwa kaburini ili kwamba
asifufuke, kwa kuweka jiwe kubwa sana mlangoni mwa lile kaburi na kisha kulipiga 'muhuri' ili atakayeligusa tu akamatwe na kufungwa gerezani. Hawa walisema ‘Yule mjanja aliwahi kusema atafufuka baada ya siku tatu’ pamoja
na jitihada zao zote, ilipofika siku ya
tatu, 'malaika kijana wa Bwana' aliliviringisha lile jiwe lao na kwa dharau kubwa akalikalia, na wale walinzi wakawa 'kama wafu'.
MAOMBI:
Walionilinda kwenye kifungo, wawe kama wafu kwa Jina la Yesu. Mlinzi yeyote aliyenilinda kwa muda mrefu uwe mfu, kwa jina la Yesu. Walinzi wote walionifunga na kusimamia hicho kifungo, leo nawatangazia kuwa Yesu ana haja na mimi, kwa Jina la Yesu. Amen |
Yamkini umekuwa kwenye kifungo kwa muda mrefu sana. pengine umeenda makanisani
kuombewa bila mafanikio. Lakini kumbe kifungo chako kimewekewa mlinzi anayesimamia kifungo
ili kwamba usipate kupenya. Siri kubwa ni wewe kumshambulia 'mlinzi' wa kifungo chako awe kama mfu katika Jina la Yesu.
MAOMBI:
Leo ninaupokea upanga wa rohoni, wenye uwezo wa kuwaua walinzi wote walionilinda nikae kwenye kamba. Kwa Jina la Yesu, nautumia upanga kuwafyeka walinzi wote walionilinda kwenye kifungo cha balaa, mikosi, umaskini Kwa Jina la Yesu. Amen
|
Walinzi wanakuwa wakikufuatilia popote uendako. Hata kama utapanda ndege uende nchi
mbalimbali ikiwemo Nigeria ili kuombewa, kifungo hiki hakiondoki kwa sababu ya hawa walinzi.
Leo Yesu amekuja kuzikata kamba hizo na
hao walinzi wanaokulinda wataaibika kwa
Jina la Yesu. Kwa kujua uwepo wa hawa walinzi, Yesu aliwaambia wanafunzi
wake, wawambie hao walinzi wa punda na mwanapunda “Yesu ana
haja naye”. Sababu kuu kwetu kwenye
maombi ya siku ya leo ni kuwa: “ Yesu ana haja naye…. Endapo ni ndugu yako
amefungwa, utakapomfungua leo waambie walinzi kuwa “Yesu ana haja naye”.
Wakati amefungwa, mwanapunda alikaa pale katika hali isiyomfanya mwingine amuone wa thamani yoyote.
Ndivyo inavyokuwa kwako endapo umefungwa. Yule mwanapunda alipofunguliwa na kuletwa kwa Yesu, watu walianza kuona umuhimu wa yule mwanapunda,
wakatandika nguo zao chini ili mwanapunda apite juu yake huku Yesu akiwa amekaa juu yake. Hata wewe utakapofunguliwa kwa kukatwa kwa
kamba zilizokufunga, wale ambao walikuwa hawakuoni wanaanza kukuona kwa namna
ya tofauti, na utashangaa wanaanza kukusifia.
Mordekai katika Biblia aliwahi kukaa katika hali ya
aina hii. Hamani aliwahi kumkasirikia
sana Mordekai na hata akaomba ushauri kwa mke wake wa jinsi ya kumtenda vibaya Mordekai. Ndiyo
maana ni vizuri sana mke kutoa ushauri
mzuri kwa mume wake siku zote. Mke wa Hamani
alimshauri mumewe atengeneze 'kitanzi' cha kumuulia Mordekai lakini baada ya maombi
ya kufunga kwa Wayahudi wote yakiongozwa na Malikia Esta, kitanzi kile kile
alichoandaa Hamani kilitumika kumuulia yeye mwenyewe badala ya Mordekai.
Leo ni siku
ya kuheshimishwa kwa Jina la Yesu. Katika ISAYA 43:4…[Kwa kuwa ulikuwa
wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu
hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako.]… Unapoletwa
kwa Yesu, wale wale waliokudharau wanaanza kukuheshimu kwa Jina la Yesu. Hata
hivyo huwezi kuipata heshima kama Yesu hayupo ndani yako.
Baba (SNP Dr. Godson) akimuhoji Amani, aliyekuwa Mganga wa Kienyeji, baada ya kusalimisha mkoba wake leo hapa kanisani, huku mamia ya watu wakishangaa. (Fuatana nasi kwenye hii Blog, tutakapokuletea Ushuhuda mzima wa Mganga Amani) |
Ni nafasi muhimu leo kumpa Yesu
Kristo maisha yako kwa kuokoka. Amen
© Information Ministry
(Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Kihonda VETA, Morogoro.
/or
Contact our Senior
Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757
550878 / +255 719798778
Email: godson.issa@yahoo.co.uk