Sunday, March 15, 2015

KUZIMU WANATOKA, JEHANAMU HAWATOKI-Na: ADRIANO MAKAZI (RP)


JUMAPILI:  15 MARCH 2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO


Utangulizi: Jumapili ya leo, Somo letu linaitwa Kuzimu wanatoka, Jehanamu hawatoki”. Shetani amejikusanyia watu wengi kuzimu kwa lengo la kuiniga nao jehanamu. Jehanamu ni moto alioandaliwa tayari ibilisi na malaika zake. Hadi sasa hakuna mtu ambaye keshapelekwa jehanamu, bali wote  waliokufa wapo kuzimu wakisubiri siku ya mwisho ya hukumu.


 

         1.         JEHANAMU JINSI ILIVYOANDIKWA KATIKA BIBLIA

MATHAYO 5:21-22….[Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. 22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.]…. Biblia imeitaja jehanamu  hii ya moto.

 

MATHAYO 5:29-30…[Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. 30 Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.]…Mtu anaweza kutupwa jehanamu.

 

MATHAYO 10:28…[Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.]….

 

MATHAYO 18:9…[Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum ya moto.]….

 

MATHAYO 23:15….[Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.]….

 

MATHAYO 25:41…[Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;]… Jehanamu ya moto imewekewa kwa ajili ya shetani na  malaika zake.  Jehanamu haikuanadaliwa wanadamu.

 

UFUNUO 20:10…[Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.]….

UFUNUO 20:15…[Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.]…. Vipo vitabu viwili: Kitabu cha Uzima na Kitabu cha Mauti. Wasiookoka wote wapo  katika kitabu  cha mauti, na wale waliookoka majina yao yapo katika kitabu cha uzima. Kitabu hiki cha uzima wa milele kinaandikwa na malaika,  na si wanadamu.



 

         2.         KUZIMU JINSI ILIVYOANDIKWA KATIKA BIBLIA

Ni shimo la giza amabapo ni makao makuu ya shetani. Kuzimu kama  ilivyo mbingu,  nayo imegawanyika. Je, tunajuaa je kuwa mbingu imegawanyika?

 

2KORINTHO 12:1-4…[Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia maono na mafunuo ya Bwana. 2 Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. 3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua); 4 ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.]… Mbingu ya tatu iliyoongelewa hapa ipo juu,na siyo chini. Mbingu ya tatu ndipo akaapo Mungu, na siku moja ututaenda pale. Lucifer alikuwa nakaa mbingu ya kwanza na ya  pili,  na ndiyo maana alitamani aende kukaa mbingu ya tatu kwa mujibu wa maandiko.

 

UFUNUO 9:11…[Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.]…Lucifer ndiye mkuu wa kuzimu. Kuzimu  ina malango (gates) yake.

 

UFUNUO 9:1…[Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu.]….. Kama kuna ufunguo wa  shimo la kuzimu, maana yake wapo wanaokaa humo, wanaolinda na kulimiliki. Huyu anayelimiliki hili shimo anaamuru  nani  aingie huko.

 

ISAYA 14:12…[Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!]…

 

UFUNUO 12:7-9…[Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.]… Ni nani aliyeshushwa hadi kuzimu? Shetani  aliyekuwa malaika wa ngazi ya  kerubi, akiitwa Lucifer, akikusanya sifa za watakatifu na kuzipeleka kwa Mungu. Alipoacha makao yake yanayomhusu kwa kutamani kutawala mahali pa Mungu, ndipo alipotupwa  nje.

 

UFUNUO 9:2…[ Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni. 3 Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi.]…..

 

Mtu anapokufa akiwa ameokoka, anaenda moja kwa moja paradise, mahali pa mapumziko. Endapo mtu anakufa kabla ya kuokoka, huingia kuzimu. Mfano wa kuzimu ni sawa na selo ya magereza, ambapo mhalifu yeyote huwekwa kabla ya kesi yake kuhukumiwa.

 

Jukumu letu  kama Ufufuo na Uzima ni  kuhakikisha kuwa jehsanamu anaingia shetani  tu  na malaika zake na suoyo wanandanuy walioumbwa kwa sayura na mfano wa Mungu.

 

LUKA 16:23…[Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.]….

 

Wito wetu ni  kuyafungua mashimo yote ya mashetani na kuwaweka wote walioshikiliwa hhumo  kwa Jina la Yesu.

 

LUKA 16:25…[Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.]….Kuzimu wanateswa, ni mahali ambapo waliopo kule wanaumizwa. Kumbe ukiwa kuzimu (baada ya kufa) bado akili ya mtu inafanya kazi, hata kuweza kuweka kukumbuka mambo. Kumbe waliopo paradise wanafarijiwa.

 

LUKA 23:43…[Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.  ]….Peponi ni mahali wamapokaa watakatifu wakisubiri watakatifu  wenzao hadi siku ile ya hukumu itakapowadia.

 

Kuzimu  ni roho iliyotengenezwa kwa mfumo washimo. Na ipo siku kuzimu nayo itatupwa jeheanamu ya moto.

 

MATHAYO 12:40…[Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.]…Kuzimu nayo  inafahamika kama “Moyo wa Nchi”.

 

1PETRO 3:18…[Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa,  19 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri;]...Yesu alishuka kuzimu katika zile siku  tatu na  kuzifuata funguo za mauti na kuzimu. Alikabidhi funguo hizi kwa kanisa.

 


Maandiko kadhaa wa kadhaa yanathibitisha kuwa kuzimu  watu wanatoka. ZABURI 30:3…[]… Nafsi,fahari,wadhifa,  vitu vya mtu vyaweza kupelekwa kuzimu. Yawezekana mkono wako, nafsi, macho au miguu yako imepelekwa na kuungamanishwa na kuzimu bila wewe kuwa na habati.

 

ISAYA 14:11…[Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika.]… Ina maana fahari ya mtu yaweza kupelekwa kuzimu. Fahari ni nini? LUKA 4:5-6….[Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.]… Mungu amekuumba mtu mwenye heshima, na wajanja wachache wanaibia hii fahari na kushusha hadi kuzimu.

 

ZABURI 86:13….[Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.]….

 

ZABURI 16:10…[Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.]…. Kilichopelekwa kuzimu chaweza kurudishwa.

 

ZABURI 49:15…[Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu, Atanitoa mkononi mwa kuzimu, maana atanikaribisha.]… Maana yake kuzimu yaweza kuachia.

 

MATENDO 2:27…[Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu.]…..

 

UKIRI
Imeandikwa “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure”. Leo Bwana ufufue kama ulivyosema, uwapooze wagonjwa kama ulivyosema, uwatakase wakoma kama ulivyosema, na uyatoe mapepo  kama ulivyosema, kwa Jina la Yesu. Amen.
 

 


Hapa duniani waliwahi kuwepo  watu wanaoyfanaya mashimo ili kuwwazuia watu wakae humo. Mtu awekwapo shimoni,  chochote alichokuwa anakifanya mtu hupeperuka. Mtu huanza ujenzi wa nyumba lakini mwishowe haimaliziki. Hizi ndizo dalili za walioshikiliwa mashimoni. Mbaya zaidi wewe bila kujua unamshirikisha huyo mtu mambo yako yanapaharibika ukitaka ushauri wake, kumbe anakusikiliza tu na moyoni anakiri kuwa lile jambo alilokutendea limefanya kazi sawasawa.

 

Wachawi, wasoma nyota, wapiga ramli wamevaa nia ya kumtumikia shetani.  Yapo mashimo yanayoshikilia watu.

 

UKIRI
Mashimo yoyote yanayonihusu nayawashia moto na kuyateketeza malango yake na makomeo yake kwa Damu ya  Yesu. baba wa mbinguni ninakuja kwa Jina la Yesu, nakuomba leo Bwana nipate wokovu wako, kwaJina la Yesu, kila mamalka yoyote iliyonikamata na kuniweka chini, nakataa kuwa mgonjwa, nakataa kuwa kwenye mateso, nabomoa madhabahu iliyonishikilia  kwa Damu ya Yesu, mahali popote nilipowekwa kwa namna yua uchawi, leo napabomoa kwa Jina la Yesu.  Ninavunja leo vifungo vyote nilivyofungwa na watu wa karibu, vifungo vya utasa, vifungo vya umaskini, leo navivunja kwa Damu ya Yesu. Amen
 


 
Wana wa Israeli walikaa utmwani miaka 70 na miaka 430 kwa vipindi tofauti tofauti baada ya kumuacha Mungu na kuasi.  Dhambi ni sababu ya watu kuwekwa na shetani kuzimu. Wokovu ni lazima ili shetani  asipatae fursa ya kumuweka mtu kwenye mashimo ya  mateso yake.
Share:
Powered by Blogger.

Pages