Monday, April 20, 2015

HISTORIA YA MAISHA YANGU-Na: BRYSON LEMA (RP)


 

SEHEMU (A)  MANENO YA BABA Dr. GODSON (SNP)


WAKATI WA MAPOKEZI YAKE MKUNDI MOROGORO

JUMAPILI (19/4/2015) 


 
Dr. Godson (SNP) akimtambulisha binti toka Ufufuo na Uzima Japan mara baada ya mapokezi Rasmi kwa Baba ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Mkundi Morogoro tarehe 19/4/2015.
 
 
ALICHOKISEMA BABA YETU, Dr. GODSON (SNP)

Unaposoma katika  ISAYA 40:28-31, unakutana na maneno haya ya Mungu….[Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki. 29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. 30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; 31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.]…Asomaye maneno haya na afahamu nini Roho wa Bwana awaambia watu wa Tanzania. Bwana Yesu alikamatwa, akapigwa, akatundikwa msalabani, watu wakalia na wengine wakawaza kwamba imekwisha, lakini ghafla baada ya siku tatu watu wale wale waliomtesa wakamuona tena.
 
ISAYA 22:5…[Kwa maana siku ya kutaabika, siku ya kukanyagwa, siku ya fujo inakuja, itokayo kwa Bwana, Bwana wa majeshi, katika bonde la Maono; inabomoa kuta; na kuililia milima.]… Haya yalikuwa maono niliyoyaona binafsi.
 

 
SEHEMU (B)  JUMAPILI: 19 APRILI 2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
 
SOMO: HISTORIA YA MAISHA YANGU

Na:   BRYSON LEMA (RP)

Utangulizi: Historia ya Ukristo inaonesha kuwa ulianza kwa vurugu,  na bila vita Ukristo haupo. Kila mtu ana historia yake. Katika maisha ya kila siku,yapo mambo uliyotaka kuyafanya lakni  hujaweza kuyafanya,  pengine kwa kukosa uwezo, au kukosa watu wa kukusaidia kufanya hivyo.  
 
YOHANA 5:2-6..[Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano. 3 Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke. 4 Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.] 5 Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane. 6 Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?]… Unapoangalia maisha yako, unaona kwamba kuna kitu unachokihitaji ili uingie mahali fulani. Wakati mwingine zipo sababu au watu waliofanya wewe uwe kama ulivyo: waliosababisha ndoa kukosa amani, uwepo  wa magonjwa,  kutokusoma, kufukuzwa nyumbani n.k. Wanadamu mara zote hupenda kupeleka lawama zao kwa wale waliosababisha maisha yao kuwa jinsi yalivyo.

 
Sehemu ya umati wa Majeshi ya Bwana Mkundi-Morogoro, Jumapili 19/4/2015.

Yusufu ni miongoni mwa watoto 12 wa Yakobo. Ndugu zake Yusufu walimchukia sana,kwa kuwa Baba yao  alimpenda sana Yusufu kuliko wao, na hata akamshonea mavazi yenye rangi tofauti na wao. Wakati Yusufu anawahadithia ndugu zake ndoto alizo nazo, wao kumbe jambo hilo lilikuwa linawaumiza ndugu  zake. Baadae kaka zake wakapanga kumuua ili ndoto za Yususu zisitimie.


Siku moja Baba yao alimtuma Yusufu kwenda kuwaangalia ndugu zake wakiwa malishoni, na walipomuona kwa mbali wakaweka kikao cha ghfala cha kumuua Yusufu. Bila yeye kujua, Yusufu alikamatwa  na ndugu zake wakamtupa shimoni. Hata hivyo, Mungu alikuwa upande wake. Mungu alijua kuwa bila Yusufu kuuzwa Misri, siyo rahisi kwake kutawala. Yusufu akiwa Misri zile ndoto  haoti tena,  hamsikii Mungu akiongea naye tena. Aliwekwa jela kwa kesi ya kusingiziwa, na humo gerezani alijua ndiyo mwisho wa maisha yake.

 

Yamkini wewe unaweza kusema hajawahi kutupwa shimoni  kama Yusufu na kwa hiyo hili somo halikuhusu. Kumbuka kwamba, "Agano la Kale ni la mwilini", lakini "Agano Jipya ni la rohoni". Si ajabu wapo ndugu zako ambao wamekwisha kukuweka shimoni kama Yusufu (katika ulimwengu wa roho) lakini wewe upo tu bila kufahamu kinachoendelea rohoni.

 
Siyo rahisi kumiliki bila kuingia jela. Kanisa la Ufufuo  na Uzima Duniani imepitia vipindi vyote kama Yusufu. Cha kukumbuka hapa ni kuwa Baada ya jela, kumiliki, baada ya jela kutiisha, baada ya jela kutawala. Huu  ni mwaka wa kumiliki, kutiisha na kutawala. Jela palikuwa mahali pa mateso, lakini lipo  tumaini baada ya jela. Wote waliomtuaminia Mungu waliingia jela lakini baadae wakatoka wazima.

 

Shetani lazima ajue kuwa ile miaka aliyoiiba kwako atairudisha yote. Farao aliyekuwa anawazuia Israeli wasiondoke, hatimaye ndiye huyo huyo aliwaambia waondoke na chochote wanachokitaka, ikiwemo mali na dhahabu za Wamisri. Wana wa Israeli hawakuishia jangwani bali walifika Kanaani,  maana Bwana wa Mabwana alisema, na "yeye si mwanadamu hata aseme uwongo". Ndugu za Yusufu walitummika ili kumfikisha Yusufu kwenye hatima ya ndoto yake ya kutawala. Yusufu hakuwachukia ndugu zake.  Hata wewe wale waliokuharibia maisha yako,usiwachukie kwa sababu Mungu aliwaweka mahsusi kwa ajili ya  kuinuiliwa  kwako.

 

MWANZO 45:1-8..[Hapo Yusufu hakuweza kujizuia mbele yao wote waliosimama karibu naye. Akapiga kelele, na kusema, Mwondoeni kila mtu mbele yangu. Wala hakusimama mtu pamoja naye, Yusufu alipojitambulisha kwa nduguze. 2 Akapaza sauti yake akalia, nao Wamisri wakasikia. Watu wa nyumba ya Farao nao wakasikia. 3 Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ndimi Yusufu; baba yangu angali hai bado? Wala ndugu zake hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu mbele yake. 4 Yusufu akawaambia ndugu zake, Karibuni kwangu; basi, wakakaribia. Akasema, Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri. 5 Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu. 6 Maana miaka hii miwili njaa imekuwa katika nchi, na iko tena miaka mitano isiyo na kulima wala kuvuna. 7 Mungu alinipeleka mbele yenu kuwahifadhia masazo katika nchi, na kuwaokoa ninyi kwa wokovu mkuu. 8 Basi si ninyi mlionipeleka huku, ila Mungu; naye ameniweka kama baba kwa Farao, na bwana katika nyumba yake yote, na mtawala katika nchi yote ya Misri.]… Bila ndugu zake Yusufu kumuuza Misri,  leo hii historia ya Yusufu isigekuwa inafahamika. Hakuna Samweli  bila Penina. Pale Penina anapoinuka, Samweli huzaliwa.  Wale waliokuinukia ni kwa ajili  ya ushindi wa maisha yako.

 
Hapa juu  ni Vijana wa Showers of Glory kama kamera yetu ilipowanasa wakiimba na kumchezea
Bwana wa Mabwana wote, Mungu Mkuu kuliko miungu yote - Jumapili 19/4/2015.

Wewe ambaye hujaokoka, ni vyema leo kufanya hayo maamuziilikumpata Mungu aliye mkuu kulikomiungu yote anayewatoa watu gerezani na kuwaweka katika utawala.

 
                                  © Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi, (Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
 /or
Contact our Senior Pastor:

 Dr. Godson Issa Zacharia

 (Ufufuo Na Uzima – Morogoro)

Cellphone: (+255) 757 550878 / +255 719798778

Share:

Related Posts:

Powered by Blogger.

Pages