JUMAPILI: 14 JUNE 2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi:Katika
Kitabu cha Ayubu 31:35imeandikwa ...[Laiti
ningekuwa na mtu wa kunisikia! (Tazama, sahihi yangu ni hii, Mwenyezi na
anijibu); Laiti ningekuwa na hayo
mashitaka yaliyoandikwa na adui yangu! ]…. Unapoyaangalia maisha yako ya kila
siku, ikiwemo ndoa yako, afya yako, biashara zako n.k. unaweza kukosa
majibu, lakini maswali kuhusu kinachotokea yapo pale pale. Ayubu pamoja na kuwa
mkamilifu mbele za Bwana, lakini hata
hivyo alijikuta akipata taabu, misiba na mateso mbalimbali bila kujua aliyemshataki
ni nani na mashtaka yake ni yapi.
Bila kuwepo kwa mshataki huwezi kupelekwa mahakama
yoyote ile, au kwa balozi wa nyumba kumi
mtaani mwako. Katika Biblia, shetani
anaitwa ni mshataki. Mfano: UFUNUO 12:10…[Nikasikia
sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu
wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu
zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.]….
Unapaswa kufahamu kuwa wewe kama masihi wa Bwana unaye mshtaki, naye ni shetani.
Kesi yoyote ile huanzishwa na mshtaki. Kinachofuata ni taratibu za kuwa na polisi
na wapelelezi wakiaangalia mashtaka uliyotuhumiwa nayo.
Kwa haraka waweza kuona kuwa mfumo wa serikali za
dunia hii umeundwa kwa mpango wa kishetani. Unapoona mshtaki, ujue katika
ulimwengu wa roho yapo mashtaka, mahakimu,
mapolisi na mfumo wote wa kimashtaka. Endapo
utashatakiwa huko kwenye Mahakama za kishetani unakuwa umebadilishwa jina na
kuitwa ‘mtuhumiwa’. Vita huibuka kwa sababu katika mahakama za kishetani,
wanakuwepo walinzi wanaopewa kazi ya kukulinda ili usiweze kusonga mbele. Pengine
mshtaki wako anachukizwa tu na maombi
yako hapo mtaani mwako na ambayo yanaharibu kazi zao za giza. Kwa hiyo mwisho
wa siku, mashetani yanakuwekea ulinzi usipandishwe cheo au usifanikiwe n.k. kumbuka yote haya siyo kwa sababu Bwana hapendi ufanyiwe hivyo bali
ni kwa sababu ya uwepo kwa mahakama za kishetani zenye kuwaweka watu magerezani
kwao.
Mashetani yana aina mbali mbali za vifungo. Wengine hufungwa ili
wasipate kazi, na kama hujaifuatilia ile mahakama ya kishetani yenye kukuhukumu usipate kazi basi hutaweza
kufurukuta kamwe. Vifungo vingine ni kwenye ndoa au biashara n.k.
Vifungo vyote hivi huanzia katika ulimwengu wa roho. Kwani maandiko matakatifu yanasemaje? Baadhi ya mifano
ya Kibiblia ni hii ifuatayo:
1. Kumbuka
Mungu alimwambia Yeremia “Kabla hujakaa tumboni mwa mama yako nalikujua”. Je,
kabla Yeremia hajaingia tumboni alikuwa wapi? Alikuwa katika ulimwegnu wa roho.
2. Utawaona
wale mamajusi wa mashariki, waliokuja Jerusalemu kuifuatilia nyota ya Yesu
Kristo alipokuwa amezaliwa. Je, safari ya hawa mamajusi ilikuwa ya siku moja? La
hasha. Kumbuka kuwa enzi hizo hazikuwepo ndege za kasi ili kusafirisha watu kwa haraka namna ile. Maana yake
ni kuwa, nyota ya Yesu ilishaonekana pengine miaka mitatu kabla ya Mariamu kuwa
mjamzito. Hii inadhihirisha kuwa hata
mafanikio yako katika ulimwengu wa roho
yameshaonekana, na ndiyo maana mashtaka
hupelekwa kwa mashetani ili kukuzuia.
3. Kumbuka
pia kuwa kabla ya Musa kuzaliwa hali ilikuwa shwari. Lakini kipindi kile cha
kukaribia kuzaliwa kwa Musa, ndipo Farao na Wamisri walianza harakati za kutaka
kuwazuia Israeli wasiondoke wala kuwa na mkombozi wa kuwavusha kwenda kwenye
nchi yao ya ahadi.
Inapokaribia wakati wakuondoka hapo ulipo kwenda
asehamu iubngunbe vita huchachamaa, na
washtaki hukaa kila upande ili kukuzuia.
Hii ni kwa sababu katika mahakama za kishetani
hiyo hujulikana mapema tu. Kumbuka kuwa kila jambo na wakati wake. Mungu ameuweka
wakati wako wa kuinuliwa. Wakati huu ukeshasogea, mashtaka na vita huongezeka.
DANIELI
6:4-5…[Basi mawaziri na maamiri
wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya
ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu,
wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake. 5 Ndipo wale watu wakasema,
Hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli huyo, tusipoipata katika mambo ya
sheria ya Mungu wake.]….Washtaki wa duniani nao hukaa ili
kutafuta makosa. Nguvu ya mshtaki iko kwenye mashtaka. Inabidi ujue kuwa pale msalabani ulipata msamaha wa dhambi
zako na hati zote za mashtaka zilifutwa.
Vipoaina mbili za vifungo.kifungo cha ndani na kifungo cha nje. Kifungo cha
ndani shetani hukaa ndani ya mtu. Huyu akiombewa mapepo ndani mwake hutoka. Kifungo cha nje ndicho kigumu sana kwa sababu
shetani hakai ndani ya mtu, ila huweka vizuizi mahali. Mathalani, mtu wa aina hii
hata akiombewa halipuki mapepo kwa
sababu mapepo hayapo ndani mwake. Badala yake, mapepo ya kumlinda yapo nje ya
mwili wake ili kuzuia na kusimamia aina hii ya kifungo alichowekewa
mtu huyu. Mathalani, mtu amehukumiwa katika
mahakama za kishetani ili apate ajali na miguu yake ikatwe, na hivyo mtu wa
aina hii apatapo ajali miguu yake itakatwa kwa sababu ya hukumu iliyoamuriwa.
Leo ni siku ya kumfuatia mshatka na mashtaka yake. Kila
adui aliyensihtaki, leo nakupiga wewe na washtaki wako wote. Lazima ieleweke
kuwa wewe una mamlka kuliko yeye. Sisi tunaye mwakili ambaye ni Yesu Kristo
aliyetupa uwezo waw kuangusha kila kazi ya kishetani. Imeandikwa “wewe
ni rungu la Bwana na silaha za Bwana za vita”. Adui zangu
mnaponiwangia nyakati za usiku na kupita angani, tutakutana huko
huko,ila tofauit yangu na ninyi ni kuwa kwenu
muda huo huo kama mwali wa moto, kwa kuwa imeandikwa “Bwana huwafanya watumishi wake
kuwa miale ya moto”. Leo siji kwenu kama mwanakondoo tena, bali
ninakuja kwenu kama mwali wa moto. Ule ukristo wa kupigwa shavu la kulia na
kugeuza uso ili upigwe shavu lingine ulishapitwa na wakati kwa sababu kizazi
hiki kimezidi uovu kupitiliza. Leo nitakupiga
wewe mchawi na mkoba wako wa uchawi. Nitaidondosha minyororo mliyonifunga kwa miali
yangu ya moto. Mlikuja kwangu na mikuki na silaha zenu lakini mimi nakuja kwenwana
wa Majeshi.
Wengi wa watu hawjui manuizo. Kwa kawaida manuizo si
shetani bali ni nguvu ya kishetani. Mfano,
shetani anaweza kuweka hali fulani ya kishetani na ambayo huwa katika kifungo ili kwamba mtu awe na maisha
wanayotaka wao. Kama uonavyo wafungwa magerzani, pia wapo wakristo waendao
makanisani lakini ni wafungwa na wapo magerezani bila wao kujua. Wakienda makanisani
huridhika waambiwapo, “Nendeni kwa amani” na kumbe warudipo majumbani
mwao, bado maisha yao, ndoa zao, na kila
wakifanyacho vimewekewa kuta ambazo haziwaruhusu kupita. Lazima uffahamu
kuwa, tatizo ulilo nala ni gereza la
kishetani. Wallinzi wa kusimamia haya mashtaka hukuzuia pande zote ili mtu wa aina hii asiweze kupenya. Leo hii tunaye
Yesu Krsito na malaika wa vita ili kufuatilia kila aina za kuta na vizuizi
vilivyowekwa na mashetni,na ni lazima nipite kwa Jina la Yesu.
Mashtaka ya kishetani huongeza kwa sababu
yamenuiziwa nguvu za kishetani. Pengine mashtaka
yako yansema ‘Hakikisha haolewi’, ‘Hakikisha ndoa yake haina amani’ ‘Hakikisha watoto wake hawasomi’ ‘Hakikisha hafanikiwi kwenye biashara yake’ n.k.
Wasimamizi wa mashtaka hukaa mkao wa kuhakikisha kuwa, kile kilichonuizwa juu
yako kinatokea vilevile.
Shetani anapokushtaki huandikisha hati ya mashtaka. Imeandikwa katika 1 NYAKATI 4:33…[na vijiji vyao vyote
vilivyoizunguka miji iyo hiyo, mpaka Baali. Hayo ndiyo makao yao, na hati ya
nasaba yao wanayo.]… Hati
ya nasaba ni sawa na kusema vinasaba (DNA). Hii ni hati ya damu ya mtu husika. Kwakawaida
hayupo mtu anayeweza kumshaatki mtu au kumchhukua msuskule asiyekuwa na damu
naye. Unaweza kufungwa kwa sababu yupo mtu aliyekamata hati ya nasaba ya ukoo
wako. Katika mila za kiafrika, mzee
waukoo anakuwepo mwenye umri mkubwa kuliko wote na ambaye mara zote hata
akienda waganaga wa kienyeji huenda kwa
niaba watu wa ya ukoo wote. Baba wa ukoo
afanyapo haya haendi kama yeye bali kama
mkuu wa ukoo wake.
Pengine hujawai hujiuliza maswali haya: Ni kwa
nini baadhi ya
makabila Tanzania huwasimika viongozi
wa kisiasa na kuwafanya machifu wa kabila lao, na kuwapa mkuki, ngao na kuvishwa
ngozi za wanyama? Fahamu ya kuwa kwa kawaida, uchifu hautolewi bila kufanyika
kafara. Maana yake ni kuwa, kafara za wanyama hufanywa kabla ya kiongozi
mhusika kusimikwa kuwa chifu na makabila husika. Maana yake ni kuwa, kiongozi wa
aina hii, hutenda mambo kwa niaba ya
kabila lile alilosimikwa kuwa chifu wao.
Vifungo vya rohoni vipo vya aina nyingi sana. Vingine
ni vya kifamilia, vingine ni vya ukoo
wako, vingine vya serikali yako ya mtaa, au jimbo lako au vilivyosababishwa na rais wa nchi
yako. Ukumbuke kuwa kila utawala huanzia rohoni kabla ya kudhihirishwa mwilini.
Leo ni lazima uazimie kujitoa katika
magereza mliyoniweka kwa Jina la Bwana. Leo
ni lazima tutoke kwenye mashtaka yao na kwa kila jambo la kishetani
walilonifanyia kwa Jina la Yesu. Hata hivyo, endapo mtu hujaokoka siyo rahisi kuweza kumshinda mshataki wa maisha
yako. Ni vyema leo kufanya maamuzi ya kuokoka kwa kumwamini Yesu Kristo
ili awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako.
© Information
Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Church
Leadreship:
Bishop Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 765979866
/or +255 713459545