GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
UFUFUO NA UZIMA - MOROGORO
JUMAPILI: 03 JULY 2016
Laana ni mkusanyiko wa mabaya yote yanayompata
mtu: misukosuko katika kazi au ndoa n.k. laana huleta mateso mengi.
Katika KUMBUKUMBU
28:20-29 imeandikwa “Bwana atakuletea laana na mashaka, na
kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea
kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo. 21 Bwana
atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo
kwa kuimiliki. 22 Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa
kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo
vitakufukuza hata uangamie. 23 Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako
zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma. 24 Bwana atafanya mvua
ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata
uangamie. 25 Bwana atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa
njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huko na huko
katika falme zote za duniani. 26 Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote
wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza. 27 Bwana atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa
bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa. 28 Bwana atakupiga
kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni; 29 utakwenda kwa
kupapasapapasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika
njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa
kukuokoa. ). Haya ndiyo mambo
yanayowatokea wanadamu hata sasa.
Unapotumia maneno ya kinyume dhidi yako, maneno hayo hugeuka na kuwa laana. Yale unayoyaona
kwa sasa ni matokeo ya maneno uliyowahi kutamkiwa au kujitamkia mwenyewe: Hii ni kwa sababu Biblia inasema "maneno ni roho". Na
unapotaka kuwa huru dhidi ya laana, anza kwa kushughulikia chanzo cha tatizo. Chombo cha kupokelea laana yoyote ile ni
DHAMBI. Bila dhambi, laana haiwezi kukupata, na hii ni kwa sababu Biblia inasema MITHALI 26:2 “Kama shomoro katika kutangatanga
kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka
kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu
haimpigi mtu.” Laana ikikosa pa kwenda inamrudia yule anayeituma
/anayeinena.
Unapaswa kuchukua hatua kwa kumwendea Bwana nje ya lango, na Bwana atawashikisha kishindo maadui zako kama ambavyo wale wakoma wanne nje ya lango walipoleta ufumbuzi wa tatizo la njaa kule Samaria. Wapo watu waliojifungia ndani lakini wana matatizo mengi sana na ambayo chanzo cha hayo matatizo ni viumbe wa rohoni.
Unapaswa kuchukua hatua kwa kumwendea Bwana nje ya lango, na Bwana atawashikisha kishindo maadui zako kama ambavyo wale wakoma wanne nje ya lango walipoleta ufumbuzi wa tatizo la njaa kule Samaria. Wapo watu waliojifungia ndani lakini wana matatizo mengi sana na ambayo chanzo cha hayo matatizo ni viumbe wa rohoni.
Mtu unapokuwa na dhambi, laana hukaa.
Inategemea na maamuzi unayochukua katika maisha yako. Kupitia ulimi wako unao
uwezo wa kuamua hatima yako itakuwa je!!? Chagua leo kuwa na uzima ili uishi au
uendelee kuwa na dhambi upate mauti, kwa kuwa "mshahara wa dhambi ni mauti". Zipo
laana za wanadamu, laana ya Mungu, laana ya wachawi, laana ya kumuibia Mungu
zaka n.k.
BIBLIA INATUFUNDISHA AINA MBALIMBALI YA LAANA:
- Laana ya kuchonga au kuifanya sanamu. KUMBUKUMBU 27:15 “Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina).
- Laana ya Kuondoa mpaka. Wapo watu wanaoweza kuondoa mpaka wa maisha yako. KUMBUKUMBU 27:17 (Na alaaniwe aondoaye mpaka wa jirani yake. Na watu wote waseme, Amina.)
- Kitendo cha kumpotosha mtu nayo ni laana. KUMBUKUMBU 27:18 (Na alaaniwe ampotezaye kipofu akakosa njia. Na watu wote waseme, Amina.).
- Laana ya Kutowaheshimu wazazi. Hii huleta laana kwa maisha yako. KUMBUKUMBU 27:16... (Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.). Pia imeandikwa katika WAEFESO 6:1-3 (Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. 2 Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, 3 Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.). Wapo watu wengi sana wanajisahau wakeshafika mijini, na matokeo yake mabo yao hayawezi kunyooka.
- Laana ya Kudhulumu haki ya mtu. KUMBUKUMBU 27:19 (Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina.
- Laana ya Kulala na mke wa Baba yako, KUMBUKUMBU 27:20 (Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina.). Hii ni kama Reubeni alivyofanya, wakati huo mzee Yakobo alilaani kitendo kile cha Reubeni kuwa asiwe mkuu kwa kuwa aliuruka mpaka kama maji. Imeandikwa katika MWANZO 49:3-4.... (Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu. 4 Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.)
- Laana ya Kulala na wanyama. KUMBUKUMBU 27:21... (Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Amina.)
- Laana ya Kulala na dada yako. KUMBUKUMBU 27:22 imeandikwa (Na alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na watu wote waseme, Amina.). Mfano rahisi ni Amnoni mwanane Daudi aliyelala na dada yake Tamari, na mwishowe akaja kuuwa na nduguye aitwae Absalom.
- Laana ya Kulala na mkwe wako (mama wa mke wako). Imeandikwa katika KUMBUKUMBU 27:23 (Na alaaniwe alalaye na mkwewe, mamaye mkewe. Na watu wote waseme, Amina.)
- Laana ya Kumpiga mwenzako kwa siri. Hii ni kama vile kumsema mwenzako, au kumsengenya. KUMBUKUMBU 27:24 (Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina.)
- Laana ya Kuua mtu au kutoa mimba. Imeandikwa katika KUMBUKUMBU 27:25.... (“Na alaaniwe atwaaye ujira wa kumwua asiye makosa. Na watu wote waseme, Amina.”)
- Laana ya kutoshika sheria ya Mungu. Imeandikwa katika KUMBUKUMBU 27:26 “Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina”).
- Laana ya Kumlaani aliyeokoka. Hata kama wewe ni mzazi, laana ya aina hii yaweza kukurudia kwa kuwa tayari wewe umebarikiwa.
- Kutenda
kinyume na maneno ya watumishi wa Bwana. Wengi wa watu wameharibikkiwa hapa. Na
hili linathibitishwa pale ambapo mambo
fulani unayotaka yaondoke katika maisha yako lakini hayaondoki. Kuhani ni
daraja kati ya hiyo madhabahu na Mungu katika ulimwengu wa roho. Endapo utatenda
kinyume na kuhani wako au kusema vibaya juu
ya kuhani huyu ujue ni laana.
DALILI ZA MTU MWENYE LAANA
Tunajifunza kuusu hizi dalili ili kukusaidia wewe
pale unapoona mtu mwenye dalili hizo au wewe mwenywe ujue kuwa utafanya kitu
gani. Shetani ni mshataki wetu mbele za Mungu,
lakini Biblia inasema katika UFUNUO
12:11 “Nao wakamshinda kwa damu ya MwanaKondoo, na kwa neno la ushuhuda wao;
ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.” Lengo la laana ni kumzuia mtu
asiende pale ambapo Mungu amekusudia wewe kwenda.
Zifuatazo ni dalili za mwenye laana:
1.
Kutofanikiwa kwa kila
uendako.
Imeandikwa katika KUMBUKUMBU 28:16 (Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani.).
Kwa nini inakuwa ngumu kwa mtu mwenye laana kufanikwa? Ni kwa sababu unalaaniwa
mjini na unalaaniwa mashambani. Wapo wanaokimbia kufanya biashara zao mijini
wakakimbilia vijijini, lakini hilo nalo halisaidii, kwa sababu hata huko laana
inakufuatilia. Inapotamkwa baraka kwako, ni vizuri kujua ni Baraka ya aina gani
anakutamkia. Kama ni kupata watoto, na aseme “Ubarikiwe upokee watoto”
na wewe useme “Amen”.
Yupo mtu mmoja katika
Biblia ambaye alibarikiwa wakati wa kwenda na wakati wa kurudi. Huyu ni Yakobo.
Wakati wa kuondoka alibarikiwa na Isaka babaye, na kupitia Rebeka mama yake
akapata Baraka zilizokusudiwa kwa nduguye Esau.
2.
Kukosa mwelekeo (KUMBUKUMBU
28:33). Wapo watu wa aina hii, leo yupo Kanisa la Siloamu kesho yupo KKKT
n.k. Hata hivyo, kokote unapodondokea, watu wanajua hakika huyu mtu anazo
dalili za laana.
3.
Kutokupiga hatua katika maisha. Miaka nenda rudi, mtu anabaki kuwayule yule. Ukiziona dalili
kama hizi, achana na kitanda, anza
kuchukua hatua kwa kufanya maombi ya kushindana.
YOSHUA
6:1-3
... (Basi
Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Israeli; hapana mtu
aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia. 2 Bwana akamwambia Yoshua, Tazama,
nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake. 3 Nanyi
mtauzunguka mji huu, watu wote wa vita, mkiuzunguka mji mara moja. Fanya hivi
siku sita. 4 Na makuhani saba watachukua tarumbeta saba za pembe za
kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba mtauzunguka mji mara saba,
nao makuhani watapiga tarumbeta zao. 5 Kisha itakuwa watakapopiga hizo pembe za
kondoo waume kwa nguvu, nanyi mtakaposikia sauti ya tarumbeta, watu wote
watapiga kelele kwa sauti kuu; na ukuta wa mji utaanguka chini pale pale, na
hao watu watapanda, kila mtu akiendelea mbele kukabili.).
UKIRI
LEO TUNATAMKA, NA
KILA ATAKAYEKULAANI JAMBO LIWEPO LA
KUMPATA.
KWA JINA LA YESU, BWANA YESU NINAKUJA MBELE ZAKO,
NINAOMBA UNISAIDIE.
|
Unachotakiwa sasa ni kutoruhusu chombo cha
kupokelea laana kisipatikane kwako, yaani usiwe na DHAMBI. Usiwepo mlango wowote wa laana katika
maisha yako. Wewe ambaye hujaokoka leo ni siku
muhimunsanakwako kumpa Yesu
maisha yako
UKIRI
Nimepewa
mamlaka ya kuakanyaga nyoka na nge na kazi zote za yule muovu. Ewe laana
nakukanyakga kwa Jina la Yesu. Ewe ngome ya laana leo anguka kwa Jina la
Yesu. Kuanzia leo navaa alama mpya zile alama walizoniwekea ili nilaaniwe,
leo hii naweka alama mpya ili nikionekana nibarikiwe, kwa Jina la Yesu. Chapa
ya Kristo iwe juu yangu ili kila atakayeniona anibariki kwa Jina la Yesu.
Amen
|
© MEDIA &
INFORMATION MINISTRY,
GLORY OF CHRIST (T) CHURCH
MOROGORO CHURCH
|